Exodus 36:20-25

20 aWakatengeneza mihimili ya kusimamisha ya mti wa mshita kwa ajili ya maskani. 21Kila mhimili ulikuwa na urefu wa dhiraa kumi,
Dhiraa 10 ni sawa na mita 4.5.
na upana wa dhiraa moja na nusu,
Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.
22zikiwa na ndimi mbili zilizokuwa sambamba kila mmoja na mwingine. Wakatengeneza mihimili yote ya maskani jinsi hii. 23Wakatengeneza mihimili ishirini kwa ajili ya upande wa kusini wa maskani, 24na wakatengeneza vitako arobaini vya fedha vya kuweka chini ya hiyo mihimili, vitako viwili kwa kila mhimili, kimoja chini ya kila ulimi. 25Kwa upande wa kaskazini wa maskani wakatengeneza mihimili ishirini
Copyright information for SwhKC